Hyppää sisältöön

Virusi vya korona: Miongozo ya kinga dhidi ya virusi na ya matibabu ya ugonjwa huu

Koronavirus: Ohjeita virukselta suojautumiseen ja taudin hoitoon, swahili (päivitetty 13.4.2022)

Tekstit ohjausta ja neuvontaa varten:
Ohjeet suomeksi
Ohjeet englanniksi

Chanjo dhidi ya virusi vya korona

Chanjo nzuri sana zimetengenezwa dhidi ya ugonjwa wa korona.

Si lazima mtu akubali kupokea chanjo hii. Hata hivyo, chanjo hiyo inafaa kuchukuliwa, kwani inatoa ulinzi mzuri, hasa dhidi ya ugonjwa mkali wa korona, na kupunguza maambukizo ya virusi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Kurudi kwenye maisha ya kawaida zaidi ya kila siku hakuwezekani kabla ya watu wa kutosha wamechanjwa.

Manispaa na miji hupanga huduma za chanjo. Manispaa yako inakutaarifu juu ya mahali pa chanjo kupatikana na njia ya kuipata. Kwa hiyo fuatilia tovuti za manispaa au mji wako na taarifa zingine. Unaweza kuomba msaada wa kupanga miadi kutoka kwa watu wa karibu, lakini manispaa yako huweza kukupatia chanjo hata bila miadi.

Chanjo ya korona hutolewa nchini Finland kwa mtu yeyote aliye na umri wa zaidi ya miaka 5 na anayetaka kupokea chanjo hiyo.

Chanjo ya ugonjwa wa korona haikugharimu chochote.

Je, chanjo ya korona inafaa kwa nani?

 • Chanjo za korona kwa ujumla zinafaa kwa kila mtu.
 • Chanjo inaweza kuchukuliwa hata ikiwa mtu ana ugonjwa fulani. Hata matumizi ya dawa fulani haizuii chanjo ya ugonjwa wa korona kuchukuliwa.
 • Tunapendekeza chanjo kwa wanawake wote wajawazito, kwani ujauzito huwaweka hatarini kwa kupata ugonjwa mkali wa korona. Ugonjwa mbaya huongeza hatari ya kuganda kwa damu ndani ya mishipa na uwezekano wa mtoto kuzaliwa mapema kabla ya wakati mwafaka. Uchunguzi ambao tayari umefanywa na ufuatiliaji wa watu waliopata chanjo haujaonyesha wasiwasi wowote juu ya usalama kwa mjamzito au kwa maendeleo ya kijusi (mtoto tumboni). Wanawake wengi wajawazito duniani wameshachanjwa.
 • Chanjo inaweza pia kutolewa wakati wa kumnyonyesha mtoto. Vitu vya chanjo haviingii ndani ya maziwa ya mama. Mtoto pia anaweza kupata ulinzi kutoka katika chanjo ya mama.
 • Chanjo ya korona haina kitu chochote cha asili ya wanyama. Ni bidhaa inayoitwa halal na kosher na inafaa pia kwa watu wasiotumia bidhaa zenye asili za wanyama.

Unaweza kumwuliza daktari wako ikiwa chanjo za korona zinakufaa.    

Usalama wa chanjo za virusi vya korona

Watu wanaruhusiwa tu kupewa chanjo ambazo ni bora na salama za kutosha. Chanjo zinapimwa
kwa uangalifu kabla ya kuzitumia. Watengenezaji wa chanjo wamepima chanjo na maelfu makumi
ya watu wa kujitolea.

Chanjo inahitaji kupata kibali cha mauzo kabla ya kuitumia kwa wanadamu. Kibali cha mauzo
kitapewa na mamlaka ya madawa. Kibali cha mauzo kitapewa ikiwa chanjo ni salama ya kutosha na
yenye ufanisi.

Chanjo zote zinaweza kuwa na madhara. Kawaida madhara ni madogo na ya kupita haraka.
Madhara ya kawaida kwa mfano ni yafuatayo:

 • mahali ulipopigwa na sindano kugeuka nyekundu, kuvimba au kuwa na moto,
 • homa,
 • maumivu ya kichwa au maumivu ya misuli.

Chanjo za korona haziwezi kumletea mtu ugonjwa wa korona kwa sababu chanzo hizi hazina virusi hai vya korona.

Kama chanjo za kila aina, hata chanjo ya ugonjwa wa korona inaweza kusababisha athari kali ya mzio (allerginen). Athari za mzio ni nadra sana. Zinaweza kutibiwa katika vituo vyote vinavyotoa huduma za chanjo.

 • Maambukizo ya musuli wa moyo na ya mfuko wa moyo yameripotiwa zaidi miongoni mwa watu waliopokea chanjo ya mRNA kuliko mwa watu wengine. Maambukizo ya musuli wa moyo yameripotiwa zaidi miongoni mwa wanaume vijana baada ya siku chache za chanjo ya pili ya korona. Hata hivyo, maambukizo ni nadra miongoni mwa vijana, na kawaida ni kwam-ba dalili ni ndogo. Comirnaty ya Biontech-Pfizer na Spikevax ya Moderna zinahesabiwa kuwa chanjo za mRNA.

Ugonjwa wa virusi vya korona pia huongeza maambukizo ya musuli wa moyo.

Shirika la Afya na Ustawi (THL) linachapisha kwa Kifini, Kiswidi na Kiingereza habari za kisasa
juu ya madhara yanayoweza kuwa na uhusiano na chanjo za virusi vya korona. Tumia kiungo hapa
chini na kusoma habari zinazopatikana kuhusu chanjo zinazotumika sasa.

Chanjo na virusi vya ugonjwa wa korona (kwa Kifini)

Virusi vya korona vinaambukizwa kutoka kwa mtu hadi mtu
mwingine

Virusi vipya vya korona hupitishwa hasa kama maambukizo ya matone wakati mtu aliyeambukizwa
akikohoa, kupiga chafya, kuongea, au kuimba, na matone huruka kwa kupitia mawasiliano ya
karibu moja kwa moja kwenye utando wa mtu mwingine mwenye afya.
Virusi vya korona pia vinaweza kupitishwa kwa njia ya kugusana. Virusi vinaweza kuambukizwa,
kwa mfano, ikiwa mtu aliyeambukizwa anakohoa kiganjani mwake na kumgusa mtu mwingine
anayechukua usiri (maji maji) wa kikohozi kwa mkono wake kwenye utando wa kinywa au pua.

Pia virusi vya korona vinaweza kupitishwa kutoka kwa mtu ambaye hana dalili za ugonjwa wa
virusi vya korona.

Fuata hatua hizi uweze kuvizuia kuenea kwa virusi vya korona:

 • Usikae karibu na watu wengine.
 • Epuka kugusana kimwili na watu wengine. Kwa mfano, msipeane mikono, lakini tafu-ta njia zingine za kusalimiana.

Nawa mikono, kohoa kwenye mkono wa nguo

Kutunza usafi wa mikono yako ni njia mojawapo ya kuzuia ueneaji wa virusi vya korona.

 • Nawa mara kwa mara mikono vizuri na sabuni na maji. Nawa mikono hasa unapoingia ndani
 • kutoka nje, unapoanza kupika na baada ya kwenda chooni.
 • Ukishindwa kunawa mikono, tumia kitakasa mikono (dawa ya kusafisha mikono).
 • Funika midomo yako unapokohoa au kupiga chafya. Tumia, kwa mfano, kitambaa cha mkononi
 • au mkono wa nguo. Usikohoe au kupiga chafya katika kiganja cha mkono wako.
 • Usiguse macho yako, pua lako au midomo yako kwa mikono ambayo haijanawiwa.

Kunawa mikono na kukohoa (kwa Kifini)

Vaa barakoa (maski)

Ikiwa una dalili za ugonjwa wa virusi vya korona au tayari umegundulika na maambukizo ya virusi
vya korona, kaa nyumbani na epuka kukutana na watu wengine. Ikiwa nyumbani unahitaji kukaa
karibu na watu wengine, tumia barakoa.

Vaa barakoa miongoni mwa watu wengine. Vaa barakoa unapotembelea, kwa mfano, duka la
kawaida au duka la madawa, na unaposafiri kwa usafiri wa umma. Unapovaa barakoa, unawalinda
wengine wasipate maambukizo.

Unapaswa kuvaa barakoa hata ikiwa tayari umeshaugua ugonjwa wa virusi vya korona. Bado
unaweza kuambukizwa na kuwambukiza wengine.

Vaa barakoa hata kama umeshapokea chanjo ya virusi vya korona. Uwezo wa chanjo kuzuia
maambukizo ya virusi kutoka kwa mtu hadi mwingine haujulikani bado.

Matumizi ya barakoa kwa usahihi (filamu ya YouTube kwa Kifini)

Karantini na utengano

Ikiwa umepimwa korona na unasubiri majibu ya kipimo hicho, epuka kuwasiliana na watu wengine.

Ikiwa unakuwa na shaka la kuambukizwa na virusi vya korona, unaweza kuwekwa kwenye karantini rasmi. Wafanyakazi wa kitengo cha magonjwa ya kuambukiza ya manispaa au
ya mji watakupatia tarehe ya karantini kuisha. Kwenda kwenye kipimo cha korona hakufupishi
muda wa karantini.

Ikiwa unaugua ugonjwa wa virusi vya korona, unaweza kutengwa rasmi. Wafanyakazi wa
kitengo cha magonjwa ya kuambukiza ya manispaa au ya mji watakuambia tarehe ya kutengwa
kwako kuisha. Kwa sababu virusi vya korona vinaambukizwa kutoka kwa mtu hadi mtu mwingine,
unapaswa kukaa mbali na watu wengine. Pia jaribu kukaa mbali na watu unaoishi nao katika
nyumba moja. Unapaswa kukaa katika chumba tofauti kuliko wengine ikiwezekana.

Kusudi la karantini na la kutengwa ni kuzuia ueneaji wa virusi vya korona. Uamuzi juu ya karantini
na kutengwa hufanywa na daktari wa magonjwa ya kuambukiza. Ni muhimu kufuata maagizo
uliyopewa na daktari wako wa magonjwa ya kuambukiza.

Dalili za virusi vya korona

Virusi vya korona vinaweza kusababisha dalili mbalimbali. Wengine hawapati dalili zozote.
Sehemu ndogo ya wagonjwa hupata dalili kali. Dalili zinaweza kubadilikabadilika wakati wa
ugonjwa.

Dalili za virusi vya korona zinaweza kuwa zifuatazo

 • maumivu ya kichwa
 • usumbufu wa kunusa
 • usumbufu wa kuonja ladha
 • mafua
 • pua iliyojaa makamasi
 • kikohozi
 • upunguvu wa kupumua
 • kukosa nguvu
 • uchovu
 • maumivu ya misuli
 • maumivu ya koo
 • koo yenye kukwarusa
 • homa
 • kichefuchefu
 • kutapikatapika
 • kuhara

Nifanye nini ikiwa nina dalili za ugonjwa wa virusi vya korona?

Ikiwa una dalili za ugonjwa wa korona, kaa nyumbani. Ukitaka, unaweza kujipima nyumbani. 

Vipimo hivi vya korona vya nyumbani vinaweza kununuliwa kwenye maduka na maduka ya dawa.

Soma tovuti za manispaa au mji wako kwa maagizo zaidi ili ujue kwamba unahitaji kuenda kupimwa na kwamba unaomba miadi ya kipimo cha korona kwa njia gani.

Katika huduma za afya ya umma, kama vile maeneo ya upimaji wa korona ya manispaa au mji,
huduma hupatikana bila malipo. Kipimo cha korona kinaweza pia kufanywa katika huduma ya afya
ya kibinafsi, kama kituo cha madaktari wa kibinafsi. Kipimo hicho ni cha kulipa.

Unaweza pia kutumia huduma ya Omaolo kufanya makadirio kwamba dalili zako zinaendana na
ugonjwa wa virusi vya korona. Kwenye manispaa kadhaa, unaweza pia kuweka miadi kwa kipimo
cha virusi vya korona kwa kupitia Omaolo. Unaweza kutumia tovuti hii kwa Kifini, Kiswidi na
Kiingereza. Ikiwezekana, muulize mtu unayemjua kukusaidia, kwa mfano ya kutumia mtandao,
kwa kutumia huduma ya Omaolo.

Huduma ya Omaolo (kwa Kifini)

Kumbuka kwamba unaweza kuenda kwenye kituo cha afya salama ikiwa huna dalili za ugonjwa wa
virusi vya korona. Usiache magonjwa yako mengine bila kutibiwa.

Nifanye nini nikiugua?

Ikiwa dalili zako ni kali, unaweza kuhitaji kulazwa hospitalini. Ikiwa dalili zako ni nyepesi,
unaweza kuugua nyumbani.

Kumbuka mambo yafuatayo unapokaa nyumbani kama mgonjwa:

 • Kaa nyumbani na epuka watu wengine. Ikiwa nyumbani unahitaji kuwa karibu na watu wengine,
 • vaa barakoa ya uso.
 • Pumzika na tumia vinyuaji sana.
 • Ikiwa una homa, unaweza kutumia dawa za kupunguza maumivu. Kwa mfano, ibuprofeeni na
 • parasetamoli husaidia.
 • Nawa mikono mara kwa mara.
 • Kohoa na kupiga chafya kwenye mkono wa vazi au kwenye kitambaa cha mkononi. Tupa
 • kitambaa cha mkononi ndani ya takataka baada ya kukitumia.

Usitumie sehemu ambazo ni kwa wote kwenye nyumba unapoishi ukiugua.
Ugonjwa wa virusi vya korona huweza kusababisha kizibo cha mishipa ya damu. Wakati wa
kuugua ugonjwa wa virusi vya korona, wasiliana na daktari wako ikiwa unaweza kuwa na hatari ya
kuganda damu.

Virusi vya korona na elekeo la kupata kizibo kwenye mishipa ya damu (kwa Kifini)

Fuatilia hali yako. Ikiwa unajisikia vibaya, piga simu kwa kituo cha afya.
Ikiwa unahitaji kwenda kumwona daktari, tumia barakoa ya uso.

Mapendekezo na mazuio yalivyopo

Unaweza kuangalia mapendekezo na mazuio ya kisasa yaliyotolewa na mamlaka kwenye tovuti ya
Serikali.

Mazuio na mapendekezo wakati wa janga la korona (Serikali, kwa Kifini)

Angalia pia

Miongozo na mapendekezo ya virusi vya korona hubadilika, habari mpya juu ya virusi zikipatikana
au hali ya janga ikibadilika. Soma habari za kisasa juu ya virusi vya ugonjwa wa korona katika lugha mbalimbali kwenye tovutiya Shirika la Afya na Ustawi (THL): thl.fi/koronainfo

Kila siku ya kazi THL inaongeza habari mbalimbali kwa Kifini. Habari hizo zinapatikana kwa
Kifini. Habari ya kisasa kuhusu virusi vya korona (kwa Kifini)

Unaweza kuuliza zaidi kuhusu mambo yanayohusiana na korona kwa mfano kutoka kwa nesi kwenye kituo cha afya.